Change Tanzania(ns)!

Unajua tunapiga kelele about #changeTanzania, but kiukweli it starts with individuals. Tanzanians hatuna msimamo, tuko vuguvugu – we are neither black or white but grey – na tunaridhika haraka sana!

On kuridhika – umeme ukikatika miezi, mradi nina kibatari, life goes on. Maji hamna mwezi mzima, mradi we can buy, life goes on. Fuel ikiisha kwenye fuel stations for weeks, mradi I can take a cab, life goes on. Mume aki-cheat, mradi ananlisha, life goes on. Nkifukuzwa kazi bila kutendewa haki, mradi nina buzi la kuchuna, life goes on. Sina ajira, mradi kesho I can bangaiza, life goes on. Yakinzidi as a woman ntauza k na as a man ataiba. Yakinzidi sana I dump my kids with bibi vijijini na as a man nakana watoto. Ili mradi life goes on.

On the kutokuwa na msimamo na kuwa grey – jamaa kaoa but pembeni ana nyumba ndogo tatu. Binti kaolewa but ana buzi na Serengeti boy. Leo nmesimama napigania haki za wananchi as mwanachama pinzani, kesho nakaa kimya after kununuliwa. Unamkuta mama anajiita mkristu na kanisani yuko mbele mbele, mpaka magoti yamechubuka but come Saturday yuko kwa mganga Chungu Chekundu with jogoo jeusi kwapani na wikiendi anabubunya kikombe cha Babu.

Society doesn’t ask a woman unakula wapi or unalala wapi or unafanya wapi kazi? Una maendeleo gani? But instead utaulizwa unazaa lini. Society won’t ask a man unakula wapi or unalala wapi or unafanya wapi kazi? Una maendeleo gani? But instead utaoa lini.

Society haitamsema the man sleeping with a 16year old. The wife with mafiga matatu. The 16yr old found at a pub drinking. The priest with a girl at a guest house. The mjomba anayeiba. Hatusutani na kuongozana kwenye maendeleo. The mwanaume anayechafua meza sehemu sehemu but nyumbani hamna hata unga! The mwanamama aliyevaa gold mpaka kitovuni na kwenye meno but nyumbani mtoto kavaa matambara. The kaka anayemtwanga wifi mpaka jino la Christmas linatoka. The dada anayeacha watoto wenyewe usiku shemeji akisafiri, ili akalale na buzi na amchune vizuri.

We are not strong as a nation or as a people. Tunababaishwa na vitu vidogo sana! Hatuna msimamo na tu-wanafiki!

Change should start at individual level! Change starts at individual level, then it moves to group level and so forth, hii kitu ni muhimu sana regardless of which political party you belong. Upuuzi utapunguaje while mimi na wewe as a people hatuheshimu nyumba zetu, wenetu, Mungu wetu? If I can’t respect my own family, kweli wewe mtu wa nje nitakuthamini? Kenya na Zambia wameweza because first as a people na a society outlook yao ni tofauti kuliko sisi mno! Tusimsubiri rais, mbunge, mwalimu wala daktari! It should start with me and you! Tukishajifunza kujiheshimu, kujiamini, kujithamini, kujipenda na kutokuogopa ndo change will take place.

Unajua unaweza ukawa unafanya kitu bila mwenyewe kujitambua unless someone points it out. I want the best for my country na wananchi wenzangu. So kila siku nmekuwa nakuna kichwa mpaka nywele zikawa nyeupe, wondering where we could have gone wrong with a country this rich in resources etc. It might be the blonde in me, kuwa imenchukua this long mpaka leo ndo nmepata light bulb moment, nkapata jibu. But atleast I got it and said it!

As I was saying the solution ni mimi na wewe kubadilika! Mtoa rushwa na mpokea rushwa ni mimi na wewe. Mchunaji buzi na mhongaji ni mimi na wewe. Anayeenda kwa mganga Chungu Cheusi na anayetupa majini ni mimi na wewe. Mbangaizaji na muuzaji ni mimi na wewe. Mimi na wewe ni waTanzania, so mimi na wewe must change!

Wengine wata-argue tusipige kura as tumechoka CCM. Lakini, tusipopiga kura halafu? Hiyo itasaidia chochote? Tutakuwa hatujarekebisha chochote! Wakurekebisha ni sisi wenyewe! Sio Mungu, raisi, mbunge, mwalimu sijui nani – it is you and mimi! Kususa kura or kuwanunia CCM won’t solve anything!
Because of this, whomever comes next – unless he is a dictator – such, as long as we don’t change as a people, matatizo yatakuwa ni yale yale. Ataanza vizuri, and he will try hard, but atatokea Sandra atakayejaribu kumhonga ili apate a certain deal. Then atatokea Aikaruwa, then Mushi, after that ataona “schitt, I might as well join them!”

Again – the issue here ni mimi na wewe! Kama mimi as a person, as an individual ningekuwa najiheshimu, ningeheshimiwa basi na wengine. Kama ningekuwa naheshimu my place of work, my family, my place of prayer, my community etc. Na hatuna hata aibu!

But mimi ndo unaniona kwenye blogs I’m showing off gari yangu ya millions and dining at 5-star hotels daily while mshahara wangu unajulikana, na huo mshahara huufikii hata 5% ya my spendings. Mimi ndo naonekana mchana kweupe na buzi najirusha sehemu sehemu while mister kapinda mgongo kazini. Hapo kazini nmeaga naumwa. Mimi ndo naingia kwenye harusi ya sista na nyumba ndogo while wife yuko home. Na hapo ndugu zangu wanamkumbatia na kumkaribisha nyumba ndogo kwa furaha zote, na kumuita ‘shemeji’. Mimi ndo naonekana kwa mganga Chungu Cheusi while shingoni nmevaa zinga la rozari. Mimi ndo namega plot ya jirani na barabara ili kujiongezea size ya plot na nikitoka na gari langu la millions, shamelessly ninatupa empty bottles barabarani nkishamaliza kunywa maji. Who will clean after him? Na wengine kumi wakifanya hivyo atalalamikia municipal council that they don’t keep the city clean? Hongo inapokelewa because tunatoa! Tusipotoa and while tunajua haki zetu itakuwaje kwani? Mabuzi wanachunika because wanatoa. Na kadhalika.

Hembu tell me, traffic police akikusimamisha what do you do? Kuwa mkweli! Tena ukiwa una haraka I bet unatoa chai haraka haraka ili uwahi mkutanoni, huku unamalizia na, “msalimie shemeji nyumbani!”.

Right now things are like this because sisi na wao ni kitu kimoja. How and why should we expect to be treated better while wenyewe hatujiheshimu? I am sorry vitu vingi ni sisi wenyewe! If change doesn’t start with us as individuals then there is no hope for our beloved Tanzania! “Mtoto umleavyo ndio akuavyo,” na tumejilelea vibaya sana!

Halafu we always talk about accountability, this is how accountability starts nchi nyingine – says nimeajiriwa kampuni ABC, kesho niko mitaani nikalewa mpaka nikatambaa. If my company wakisikia they won’t take it lightly, because I am a representation of that company – from my behaviour, my outside appearance.

Wenzetu take everything very serious. We hardly ever do. Infact wote we have behaved quite irresponsibly in one way or another bila kujali tunamuumiza nani – in the name of being youthful and having fun. The one person anayeumia the most ni sisi wenyewe. Such accountability should start at individual level. If na sisi wananchi tukiwa accountable na wenzetu (wakubwa zetu etc) pia watuheshimu.

When wenzetu are running for a position, wanachambuliwa kuanzia family background mpaka childhood, who his friends and and what he drinks. na unachambuliwa proper! And all this is for a simple reason – how is this person as a family person? Anaheshimika? Does he support his family? And how is he in his community? Anaheshimika? Is he responsible? And how was he growing up? Because if he does then atatuongoza vizuri.

Under my email signature nimeweka as a reminder to myself that, “Be more concerned with your character than your reputation. Your character is what you really are while your reputation is merely what others think you are.”

Tuanze with me and you kwanza. My salutation ya God bless Tanzania naibadili to God bless Tanzanians.

God bless Tanzanians!

Advertisements

~ by saharasoulfood on February 12, 2012.

2 Responses to “Change Tanzania(ns)!”

  1. Hakika, let it begin with you and me.

  2. I enjoyed reading this Sandra , ni kweli all that you have said and as we all know kujirekebisha is possible , people just have to see that it is possible and that they are not all fighting against the tide. Tatizo the saying “hii nchi ina wenyewe….” pisses me off big time… wenyewe ni nani jamani …hii nchi ni yetu sisi sote , so we need to start acting like we believe it.If more and more of us stood up against corruption and the unnecessary and unacceptable conditions other fellow Tanzanians are subjected to, then we will see and feel the change. Change si lazima imsubiri mtu au system …I hear you mdogo wangu

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s

 
%d bloggers like this: